Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kibaranga katika mkutano wa hadhara, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mheshimiwa William Lukuvi amesema hili ni shamba la sita kufutwa na kuwapa wananchi na Mheshimiwa Rais katika wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji waliopewa hati ya kuyaendeleza kushindwa kutekeleza makubalino.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella amesema Serikali ya mkoa wa Tanga imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo na watahakikisha kuwa wanaweka utaratibu utakaowezesha kila mwananchi apate shamba na hati ili yaweze kuwaendeleza wananchi.
Kufuatia hatua hiyo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge inayoshughulikia ulinzi na usalama Mheshimiwa Adadi Rajab amesema watahakikisha wawekezaji matapeli hawaruhusiwi kujimegea ardhi kwa manufaa yao na badala yake mashamba hayo yaendelezwe na wananchi waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni