Polisi nchini Ufaransa wameripotiwa
kutumia mabomu ya machozi kwa mashabiki wa soka wa Uingereza waliopo
mji wa Marseille kufuatia kuibuka ghasia baada ya mashabiki hao
waliolewa kuanza kuimba mpo wapi IS.
Polisi wa kutuliza ghasia wametumia
mabomu ya machozi pamoja na virungu baada ya mapigano kutokea kwenye
baa mbili ambazo mamia ya mashabiki walikuwa wanakunywa usiku wa
Alhamis, karibu na eneo la bandari ya zamani.
Moshi wa mabomu ya machozi ukionekana katika eneo hilo
Mashabiki wa Uingereza waliolewa wakiwa kando ya barabara
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni