Watoto waliozaliwa na VVU Matumaini Dodoma, waitaka jamii kuwakumbuka
By Zainul Mzige
Imeelezwa ili kuwawezesha watoto yatima ambao walizaliwa wakiwa na Virusi vya UKIMWI ambao wanapatikana katika Kituo cha Matumaini kilichopo Manispaa ya Dodoma, Watanzania wametakiwa kuungana kwa pamoja na kuwasaidia watoto hao ambao wanaishi katika kituo hicho ili kuwawezesha kuishi mazingira bora pamoja na kupata huduma za bora za afya.
Hayo yalisemwa na Msimamizi wa Kituo cha Matumaini, Sister Maria Rosaria Gargiulo, alisema kituo hicho chenye watoto 151 wakati kimeanzishwa kilikuwa kikipokea msaada kutoka Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na TACAIDS lakini kwa sasa msaada umesimama na hivyo kuwafanya kwa sasa kuishi katika mazingira magumu.
Sister Maria alisema kuwa hali ya maisha kwa watoto hao ni ngumu na hivyo kuwataka Watanzania kuwakumbuka watoto hao ambao walizaliwa wakiwa na maambukizi ya Virusi vya UKIMWI ili waweze kupata huduma bora ambazo zitawawezesha kuishi katika mazingira bora, kupata elimu na kupata dawa ambazo zitaimarisha afya zao.
Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999, Hoyce Temu (kushoto) na mfanyakazi mwenzake Beatrice Mkiramweni wakiongozwa na Msimamizi wa Kijiji cha Matumaini, Sista Rosaria Gargiulo mara baada ya kuwasili katika kituo hicho kilichopo katika manispaa ya Dodoma karibu na Hoteli ya Mtakatifu Gasper.
“Hapa wanakuja tu watu wa hapa Dodoma mara nyingi siku za Jumamosi na Jumapili ila tofauti na hivyo hatuna msaada mwingine, watoto hawa wanahitaji faraja kutoka kwa watu wengine inapendeza kuona watu wanakuja kuwaona na kuwasaidia nao wanafurahi,
“Ukiangalia hali ya kimaisha inazidi kupanda tunafanya jitihada kujisimamia sisi wenyewe lakini tunashindwa bado tunahitaji msaada sisi tumejitoa kuwasaidia hawa watoto hata hatulipwi lakini tunahitaji sana msaada wa Watanzania,” alisema Sister Maria.
Nae Mlimbwende wa Taji la Miss Tanzania 1999 na Mtalaam wa Mawasiliano wa Shirika la Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu ambaye alifika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada ambapo alituma ujumbe kwa Watanzania wengine ambao wamekuwa hawana utaratibu wa kutoa misaada kwa wahitaji na kuwataka kubadilika.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni