.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 26 Juni 2016

RICARDO QUARESMA AIPELEKA URENO ROBO FAINALI EURO 2016

Goli lililofungwa na Ricardo Quaresma katika dakika za ziada limefanikisha timu ya taifa ya Ureno kutinga hatua ya robo fainali ya Euro 2016 baada ya kuishinda Croatia na sasa watakutana na Poland katika robo fainali.

Mchezaji huyo aliyetokea benchi aliunganisha kwa kichwa mpira alioupiga katika umbali wa yadi mbili baada ya kipa Danijel Subasic kuugonag mpira uliopigwa na Cristiano Ronaldo na kukutana na winga huyo wa timu ya Besiktas.

Katika mchezo huo walipoteza nafasi za kufunga pale Domagoj Vida na Marcelo Brozovic walipokosa kufunga kwa mipira ya kichwa huku jitihada za Ivan Perisic zikishindwa kuzaa matunda baada ya mpira alioupiga kugonga mwamba wa goli.
            Mpira wa kichwa uliopigwa na Ricardo Quaresma ukijaa wavuni mwa Croatia
                    Cristiano Ronaldo akituliza gambani mpira katika mchezo huo wa jana 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni