Akizungumza katika uzinduzi wa jumuiya hiyo, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alisema malengo ya kuwa na jumuiya za kodi vyuoni ni kuwezesha jamii kupata elimu ya kutosha kuhusu kodi kupitia wanachama wa jumuiya hizo ambao watakuwa wakipatiwa mafunzo kuhusu umuhimu wa kulipa kodi lakini pia kuhudhulia midahalo mbalimbali ambayo itakuwa inazungumzia kodi.
Alisema hatua ya kuanzisha jumuiya hizo imekuja baada ya kuwa na vilabu katika shule za msingi na sekondari nchini na sasa wakaona kuna umuhimu wa kuwa na wanachama kutoka vyuo vya elimu ya juu ili wawe mabalozi wa TRA ili kusaidia utoaji wa taarifa kuhusu kodi lakini pia na wao kutambua umuhimu wa kodi ili hata baada ya masomo yao waweze kuwa walipa kodi wazuri.
“Tulianzisha mfumo wa vilabu mwaka 2008 ambapo tuna vilabu 195 kwa Tanzania Bara na Zanzibar na katika vilabu hivyo tuna wanachama 15,520 hivyo tukaona sasa ni muhimu kuwa na wanachama kutoka vyuoni ili nao waweze kupata elimu kuhusu kodi,
“Wanachama wa jumuiya hizi watakuwa na shughuli ya kutoa elimu kwa watu wengine ambao hawana elimu ya kodi, kuandaa wataalum wa elimu ya kodi kwa miaka ya baadae na hata walipa kodi wa baadae kwani tayari watakuwa wanafahamu umuhimu wa kodi kwa maendeleo ya taifa,” alisema Kayombo.
Nae Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Kodi IFM, Amon Ojode alisema kuwa ni fursa ya kipekee kwa wanafunzi wa chuo hicho kupata nafasi ya kuwa na jumuiya ya kodi na zaidi ni wanafunzi ambao wanajifunza masomo yanayohusiana na kodi hivyo wanaamini watakuwa wawakilishi wazuri wa TRA.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni