Ziara ya Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania Saccos for Women Enterprenuers)
imezaa matunda baada ya kikundi hicho cha kina mama kufanikiwa kuingia
mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala ya biashara na Kukundi cha
Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association of Women Entrepreneurs in Comoro).
Makubaliano
hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa
na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Komoro
tarehe 14 Juni 2016. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kutafuta masoko kwa
ajili ya bidhaa za Tanzania nchini Komoro, pamoja na kukutana na
wajasiriamali wa Komoro ili kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa
mbalimbali za biashara kati ya Tanzania na Komoro.
Tukio hilo
la utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vikundi hivyo vya
Wajasiriamali akina mama kutoka Tanzania na Komoro lilishuhudiwa na
Balozi wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F.
Kilumanga. Katika hafla hiyo, Mhe. Balozi Kilumanga
aliwapongeza wajasiriamali hao kwa hatua hiyo muhimu waliofikia na kuwa
ana imani ushirikiano huo utakuwa ni wakudumu na wenye manufaa kwa
pande zote mbili. Alieleza kuwa Tanzania na Komoro zinaweza kushirikiana
katika nyanja mbalimbali za biashara na ana imani kuwa hii itakuwa ni
chachu kwa wawekezaji wengine kutoka Tanzania kuja nchini Komoro kwa
ajili ya kuekeza.




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni