Timu ya taifa ya Wales imefanikiwa
kufuzu kuingia robo fainali ya Euro 2016, baada ya Gareth McAuley
kujifunga goli na kuipa ushindi dhidi ya Ireland ya Kaskazini.
Ireland ya Kaskazini iliutawala
mchezo huo na kuidhibiti safu ya ushambuliaji ya Wales, lakini
walikosa safu bora katika ushambuliaji.
Katika mchezo huo Wales walimudu
kufanya shambulizi moja tu ambalo mpira ulifika katika goli la
Ireland ya Kaskazini.
Kipa wa Ireland ya Kaskazini Michael
McGovern alibaki akiuangalia mpira wa goli la kujifunga la Gareth McAuley
Mchezaji wa kutumainiwa wa Wales Gareth Bale akikokota mpira katika mchezo huo



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni