.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 17 Juni 2016

WAZIRI MAHIGA AMTEMBELEA BALOZI SEIF OFISINI KWAKE VUGA, ZANZIBAR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mh. Augustine Mahiga Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakipongezana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu. Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanzibar inahitaji kuwa na Viwanda vya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mali ghafi zinazopatikana nchini kupitia uwekezaji wa kudumu utakaozingatia mazingira.

Alisema Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania inapaswa kujitahidi kuitanga Zanzibar katika masuala hayo ya Uwekezaji kwa mfumo mpya ulioanza kutumiwa na Wizara hiyo hivi sasa wa Diplomasia ya Uchumi.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mh. Augustine Mahiga Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar wakipongezana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu.

Alisema Visiwa vya Zanzibar vimebarikiwa kuwa na uzalishaji wa matunda tofauti yanayolimwa na wakulima katika maeneo mengi lakini hatma yake yanaishia kuoza au kununuliwa kwa kiwango kidogo.

Akizungumzia huduma za maji safi na salama Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Wizara ya Mambo ya Nje itaendelea kuwa na jukumu la kushawishi wawekezaji wa sekta ya Maji wa Kimataifa katika kusaidia Utaalamu kwenye miradi ya Kijamii ili kupunguza kero la huduma hiyo.

Alisema uwezo wa Wataalamu Wazalendo na uwepo wa huduma hiyo hasa ikizingatiwa vingi wa visima vilivyokwishachimbwa nchini haulingani sambamba na upatikanaji wa maji ambazo bado ni ndogo mno.

Mapema Waziri wa Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mh. Augustine Mahiga alisema Diplomasia ya Uchumi itakayojikita zaidi katika uzalishaji wa viwanda utapewa msukumo zaidi kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kuingia katika uchumi wa kati na kati ifikapo mwaka 2025.

Mh. Mahiga alisema Serikali kuu inaendelea na mchakato wa kufungua Balozi zake nyengine za Nje katika nchi ambazo zina uhusiano mubwa zaidi wa Kihistoria na Zanzibar katika azma yake ya kuongeza kasi ya uchumi wa Visiwa hivi.

Alisema Zipo Balozi ambazo tayari zimeshafunguliwa hasa katika nchi za ukanda wa Ghuba na kujumuisha wanadiploasia kutoka Zanzibar watakaowajibika pamoja na kazi nyengine kuendelea kuitangaza Zanzibar Kiuchumi na kiuwekezaji.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/6/2016.


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni