.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 30 Juni 2016

WAZIRI UMMY MWALIMU, MELINDA GATES WAYAPONGEZA MASHINDANO YA MAMA SHUJAA WA CHAKULA YANAYO ENDESHWA NA OXFAM TANZANIA


Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo umiliki wa ardhi.
Dkt. Eve Marie akizungumza kwa kina ni jinsi gani Serikali na Sekta binafsi zinaweza kuwekeza katika wakulima wadogo wadogo hasa wanawake  ili kuongeza uzalishaji wa Chakula.
Muwezeshaji kutoka Forum CC Faizal Issa akielezea namna wakulima ambavyo wanaweza kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi ambayo kwa sasa yanaathiri kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji katika kilimo.
Mwanamuziki maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva Mwasiti akitumbuiza wakati wa Sherehe hizo.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni