Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la
Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar Mh.
Ayoub Mohammed Mahmoud akimpongeza Balozi Seif kwa kusaidia
kufanikisha Tamasha la Shirikisho hilo.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyuo
Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar Ndugu Juma Omar Ali akitoa
maelezo kabla ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
kukabidhiwa Ripoti ya Tamasha la Michezo ya Shirikisho hilo.
Balozi Seif akiuahidi Uongozi wa
Zahilfe kuunga mkono katika kufanikisha malengo yao ya Shirikisho
hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar.
Press Release:-
Uongozi wa Shirikisho la Vyuo Vikuu
na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar {ZAHILFE }umepata mualiko wa
kushiriki kwenye Mkutano wa Kimataifa wa masuala ya Amani ya Dunia
unaotarajiwa kufanyika Nchini Benin iliyoko Magharibi mwa Bara la
Afrika.
Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Ndugu
Juma Omar Ali akiuongoza ujumbe wa Viongozi wa Shirikisho hilo
alieleza hayo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Tamasha la Michezo ya
Shirikisho hilo iliyomalizika mapema mwezi huu.
Nd. Juma Omar alisema ushiriki wa
Viongozi hao katika Mkutano huo wa Kimataifa utaoanza Tarehe 24 hadi
27 Mwezi Agosti mwaka huu utafungua njia kwa wanachama wa shirikisho
hilo kupata uzoefu kupitia taasisi nyengine za Elimu ya juu Duniani.
Alisema mpango wa baadaye wa
Shirikisho hilo katika kujiimarisha kiajira sambamba na kusaidia
Vijana wanaomaliza masomo yao umelenga kutafuta fursa za Taaluma
katika sekta ya Uvuvi ili iwafungulie njia ya kuanzisha vikundi vya
ujasiri amali.
Alisema Visiwa vya Zanzibar
vimebarikiwa kuzunguukwa na Rasilmali ya Bahari ambayo kwa karne
nyingi zilizopita bado haijutumiwa ipasavyo tokea kuumbwa kweka
ambayo inaweza kutoa mchango wa ajira kwa kundi kubwa la vijana
sambamba na kuongeza mapato ya Taifa.
Akizungumzia Tamasha la mwaka huu la
Michezo ya Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu
Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Nd. Juma alieleza kwamba michezo hiyo
ilikuwa ya aina yake kiasi kwamba washiriki wake waliweza kutoa
burdani safi iliyoshamiri ndani ya Mji wa Zanzibar.
Alifahamisha kwamba maandalizi ya
Timu za Zanzibar kwa ajili ya mashindano ya Kitaifa ya Vyuo Vikuu na
Elimu ya Juu Tanzania nay ale ya Kimataifa yameanza rasmi ili kuwapa
muda mrefu zaidi Vijana hao wa kufanya vyema kwenye kinyang’anyiro
kinachowakabili.
Nd. Juma alielezea furaha yake
kutokana na Uongozi wa Mashindano ya Kitaifa Tanzania kuiamulia
Zanzibar kupeleka Timu Nne za Mpira wa Soka na Timu 3 za Mpira wa
wavu kwenye Mashindano hayo ya Taifa ya Vyuo Vikuu na Taasisi za
Elimu ya Juu Tanzania.
Akipokea Ripoti hiyo ya Tamasha la
Michezo ya Shirikisho la Vyuo Vikuu na Elimu ya Juu Zanzibar {
ZAHILFE } Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
alisema Serikali itaunga mkono shirikisho hilo kutokana na nia yao
nzuri ya kuanza na michezo na baadaye nguvu zao kuzielekeza katika
uchumi.
Balozi Seif aliuhakikishia Uongozi
wa Shirikisho hilo kwamba atafanya juhudi za ziara wakati atapokutana
na Uongozi wa Balozi wa China Nchini Tanzania kuomba fursa za masomo
ya fani ya Uvuvi kwa vijana hao kwa lengo la kuunga mkono mawazo yao
ya kutumia fursa za ajira katika sekta hiyo.
Alisema ziara za mafunzo ya uvuvi
ndani na nje ya nchi ni muhimu kwa vile yatafungua milango ya fursa
za ajira kwa kundi kubwa la wasomi wanaomaliza masomo yao ya
sekondari badala ya kukaa wakisubiri ajira za Serikali ambazo ni
finyu kwa wakati huu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif aliushauri Uongozi wa Shirikisho hilo la Vyuo Vikuu na
Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar { ZAHLIFE } kuendeleza michezo kwa
vile inaleta upendo, urafiki, mshikamano na hata ajira kwa Vijana.
Mapema Mjumbe wa Baraza la Wadhamini
la Shirikisho la Vyuo Vikuu na Taasisi ya Elimu ya Juu Zanzibar ambae
pia ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud
alimpongeza Balozi Seif licha ya kuwa mgeni katika ufungaji wa
Tamasha hilo lakini pia alisaidia kuona Tamasha hilo linaanza na
kumalizika kwa mafanikio.
Mh. Ayoub alisema mchango wa Balozi
Seifm kwa Shirikisho hilo umekuwa Dira na matumaini mapana kwa wana
Shirkisho hilo katika hatua ya mtyazamo wa baadaye wa Taasisi hiyo
iliyokusanya wasomi wa elimu ya Juu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
30/6/2016.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni