Mwanamke
amemshtaki Waziri wa Michezo Dk. Kenya Hassan Wario akidai fedha za
matuzo kiasi cha Sh. 400,000 za Kenya, kufuatia kuvunjika kwa ndoa
yao maiaka minne iliyopita.
Mwanamke
huyo Kaltum Dima Guyo na Dk. Wario walioana nchini Kenya lakini
walifikia maridhiano ya kutengana katika mahakama ya juu ya nchini
Uingereza mnamo mwaka 2012.
Mwanamke
huyo amedai kuwa wakati wakivunja ndoa yao, waliuza mali zao
walizochuma wakiwa kwenye ndoa ili kumaliza madeni yao.
Mwanamke
huyo pia amesema alifanya kazi katika nyumba ya makumbusho ya
Horniham Jijini London ili kumsaidia Dk. Gayo kuweza kupata ada ya
kusoma masomo yake ya chuo kikuu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni