Kapteni
wa timu ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger amefunga ndoa na nyota
wa tenesi Anna Ivanovic, ambaye amekuwa na uhusiano naye tangu mwaka
2014.
Baada
ya kupata machungu ya kutolewa na Ufaransa katika mchezo wa nusu
fainal ya Euro 2016, sasa Schweinsteiger anakila sababu ya kupata
faraja kwa tukio hili la ndoa.
Schweinsteiger
akiwa wamevalia suti ya rangi ya blue bahari, mkewe Ivanovic
alionekana mwenye kuvutia mno katika vazi la harusi jeupe, katika
harusi hiyo iliyofungwa huko Venice.
Wanandoa wapya Schweinsteiger akiwa na mkewe Ivanovic kwenye boti
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni