Watu
20 wamekufa na makumi kujeruhiwa kufuatia kugongana kwa treni mbili
za abiria kusini mwa Italia.
Treni
hizo mbili zilikuwa katika njia moja wakati zikigongana uso kwa uso,
katika eneo la baina ya miji ya pwani ya Bari na Barletta.
Waokoaji
wamekuwa wakijitahidi kuwaondoa watu waliokwama kwenye mabehewa
yaliyoharibika kutokana na ajali hiyo karibu na mji wa Andria.
Mabehewa ya treni ya abiria yakiwa yameharibika baada ya kugongana treni hizo mbili
Waokoaji wakipakia kwenye gari mwili wa mtu uliowekwa kwenye jeneza baada ya kuutoa kwenye mabehewa
Waokoaji wakiwa wanajaribu kuwanasua watu waliokwama kwenye mabehewa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni