Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeongeza muda zaidi kuimarisha
idara zake ambako imeongeza muda wa wiki moja kwa Watanzania wenye
sifa za Idara ya Masoko na Habari ili kuongoza Idara hiyo.
Awali
tarehe ya mwisho ilikuwa Julai 11, 2016 lakini kwa sasa tarehe ya
mwisho itakuwa Julai 19, mwaka huu kwa nafasi ambazo TFF imetangaza
ajira.
Lengo
hasa ni kuendana na hali halisi ya uendeshaji mpira wa miguu duniani
ambako masoko, habari na mahusiano ya Kimataifa yamekuwa funguo za
kupata rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu
popote duniani.
Pili
ni kuhakikisha rasilimali za kuendesha mpira wa miguu zinatokana na
soka na vilevile kuhakikisha wadau wanapata habari sahihi kwa wakati
mwafaka.
Kwa
nafasi za kazi TFF tembelea tovuti yao www.tff.or.tz au waandikie ili
utumiwe tangazo kwa barua pepe tanfootball@tff.or.tz
Mbali
ya kuboreshwa kwa Idara hiyo ya Masoko, pia TFF imepania kutoa
kipaumbele katika masuala ya waamuzi na wanawake kwa kuanzisha
madawati ya kudumu katika Kurugenzi ya Ufundi. Hapo awali madawati ya
wanawake na waamuzi yaliendeshwa na watumishi wa kujitolea
(Volunteers) au wa muda (Part timers).
Akizungumza
na www.tff.or.tz, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine aliamsha
changamoto mbalimbali za soka la wanawake miongoni mwanzo ikiwa ni
uibuaji na uendelezaji vipaji, Timu ya Taifa, mafunzo katika taaluma
mbalimbali, ligi za wanawake na masoko kwa bidhaaa (products) za soka
la wanawake.
Kuhusu
waamuzi, Katibu Mkuu alilielezea eneo hili kama lenye changamoto
nyingi hasa hasa katika kupata waamuzi wenye viwango vya Kimataifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni