Wapinzani
wengine wa Young Africans, katika michuano ya kuwania Kombe la
Shirikisho Barani Afrika, timu ya mpira wa miguu ya Medeama kutoka
Ghana, itawasili Dar es Salaam, Tanzania Alhamisi Julai 14, 2016 kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ), imefahamika.
Young
Africans itaikaribisha Medeama ikiwa ni mchezo wa tatu kuwania taji
hilo hatua ya makundi. Mchezo utafanyika saa 10.00 jioni Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam Julai 16, mwaka huu.
Huu
ni mchezo wa tatu kwa Young Africans katika harakati za kuwania Kombe
la shirikisho hatua ya makundi. Michezo miwili ya awali ilikuwa ni
dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria ambako ilipoteza kwa bao 1-0 kabla ya
kupoteza tena dhidi ya TP Mazembe, mechi iliyopigwa jijini Dar es
Salaam.
Mchezo
wa Jumamosi utachezeshwa na waamuzi kutoka Misri ambao ni Ibrahim
Nour El Din atakayekuwa mwamuzi wa kati; akisaidiwa na Ayman Degaish
na Samir Gamal Saad wakati mwamuzi wa akiba akiwa ni Mohamed Maarouf
Eid Mansour.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni