Timu
ya Barcelona imekubali kutoa kitita cha paundi milioni 41.7 kwa klabu
ya Valencia ili kumtwaa kiungo Mreno, Andre Gomes.
Gomes,
22, alikuwa akiwaniwa pia na Juventus kama mbadala wa Paul Pogba
anayetaka kutimkia kwenye klabu ya Manchester United.
Juventus
ya Italia ilikuwa inamuwania Gomes hadi jana, lakini hawakufanikiwa
kumnasa baada ya kuzidiwa kete na Barcelona.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni