Donald
Trump ameahidi akiwa rais atakabiliana na matukio ya vitisho
vinavyoikabili Marekani, katika hotuba yake ya kukubali kuteuliwa
kuwania urais kwa tiketi ya chama cha Republican.
Katika
hotuba yake hiyo hiyo kwenye mkutano mkuu wa taifa wa chama hicho
huko Cleveland, Bw. Trump ameahidi kuwa ghasia ambazo kwa sasa
zinaliathiri taifa la Marekani, zitamalizika mapema.
Akiainisha
namna serikali yake itakavyoendeshwa Trump, amesema dola yake
itafungua mustakabali mpya kwa Wamarekani, kwa kuweka maslahi ya
Marekani kwanza pamoja na wananchi wake wa kawaida.
Donald
Trump akiwa na mtoto wake mdogo wa kiume Barron, mkewe Melania
kushoto, pamoja na mgombea mwenza wake Mike Pence na mkewe Karen,
baada ya kumaliza hotuba yake.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni