Bosi
wa kundi la mafia la Italia Bernardo Provenzano amefariki dunia akiwa
hospitali ya gereza akiwa na umri wa miaka 83.
Provenzano,
maarufu kama "The Tractor" kutokana na ukatili wake,
alikamatwa na kufungwa mwaka 2006, baada ya kuwapiga chenga polisi
kwa miaka 43.
Provenzano
alitwaa madaraka ya kuliongoza kundi la Mafia la Sicilian mwaka 1993,
baada ya kukamatwa kwa aliyekuwa bosi wao Salvatore "Toto"
Riina.
Provenzano
alikuwa anatumikia kifungo cha maisha kutokana na kufanya mauaji
kadhaa, wakiwemo majaji waandamizi wa kesi za Mamafia Giovanni
Falcone na Paolo Borsellino.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni