Ilikuwa
kama kwenye filamu ya wafu wanaotembea, na pengine mazombi wasioweza
kutembea pale makumi ya watu walipozidisha kiwango cha bangi na
kuishiwa nguvu na kubakia kama mazezeta huko Brooklyn, Marekani.
Watu
wapatao 33 walilazwa kutokana na uwezekano wa kujizidishia dozi ya
kileo aina ya K2, ambacho ni aina ya bangi, katika eneo la Brooklyn,
Marekani.
Mashahidi
wamesema waliona makumi ya watu wakiwa wamepoteza fahamu, wakitapika,
kujisaidia haja ndogo kati kati ya barabara majira ya saa tatu na
nusu asubuhi kwenye mitaa ya Bedford-Stuyvesant.
Mmoja wa watu waliotumia bangi hiyo akiwa amezimika juu ya boneti la gari lililoegesha
Huyu naye alikutwa akiwa amezimika kati kati ya magari yaliyokuwa yameegesha
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni