Timu
ya Chelsea ya Uingereza imeanza kujiimarisha kwa kufanya usajili wa
kwanza wa kumtwaa Michy Batshuayi kwa kitita cha paundi milioni 33
akitokea kwenye klabu ya Marseille kwa mkataba wa miaka mitano.
Mchezaji
huyo wa kimataifa raia wa Ubelgiji, alikuwa katika mazoezi hii leo
baada ya klabu hizo mbili kukubaliana uhamisho huo mapema wiki hii,
wakati Batshuayi akiwa kwenye michuano ya Euro 2016.
Timu
nyingine za Uingereza za Crystal Palace na West Ham nazo zilikuwa
zinamtolea macho mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22, hata hivyo
Chelsea ilizizidi kete klabu hizo za Jiji la London.
Michy Batshuayi akionyesha jezi yake aliyokabidhiwa na Chelsea
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni