.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 24 Julai 2016

CHUI MILIA AMUUA MWANAMKE MMOJA NA KUJERUHI MWINGINE NCHINI CHINA

Chui Milia katika mbunga ya wanyama iliyopo Beijing nchini China amemuua mwanamke mmoja na kumjeruhi mwingine, baada ya wanawake hao kushuka katika gari wakiwa mbugani.

Picha za video za CCTV zilizotolewa zinaonyesha mwanamke mmoja akishuka kwenye gari na kusimama pembeni ya gari hilo, na baadaye kushambuliwa ghafla na chui huyo na kuanza kuburuzwa.

Mwanamke wa pili aliuwawa pale aliporuka kutoka kwenye gari ili kujaribu kumsaidia mwenzake na kuliwa na chui huyo.

Inasemekana tukio hilo lilisababishwa na ugomvi uliokuwa unaendelea ndani ya gari hilo na kumfanya mwanamke wa kwanza kushuka katika eneo hilo licha ya kuwepo vibao vya tahadhari.
Chui Milia akimburuza mwanamke aliyekuwa amesimama nje ya gari katika eneo la mbunga ya wanayama

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni