Maziko
yamefanyika katika mji wa Kabul kwa wahanga wa shambulizi la bomu la
kujitoa mhanga linalodaiwa kufanywa na kundi la Dola ya Kiislam (IS)
na kuuwa watu 80.
Miili
bado inaendelea kuchukuliwa kutoka mochwari huku maziko ya kwanza
yakifanyika magharibi mwa mji wa Kabul.
Mlipuaji
alilenga maandamano ya jamii ndogo ya Hazara, ambayo ni ya waislam wa
jamii ua Shia, ambayo inachukiwa na kundi la IS ambalo ni Sunni.
Rais
Ashraf Ghani ameongoza dua ya kuwaombea waliokufa na taifa la
Afghanistan limetangaza siku moja ya maombolezo ya kitaifa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni