Bondia
Deontay Wilder anataka kuzichapa na Tyson Fury na Anthony Joshua
baada ya kufanikiwa kutetea mkanda wake wa uzito wa juu wa WBC, kwa
ushindi wa KO dhidi ya Chris Arreola.
Mmarekani huyo mwenye miaka 30, alimdhibiti Arreola, kwa kumbana
vilivyo kwa makonde kwenye kona katika raundi ya nane na mchezo huo
kukoma katika raundi hiyo huko Birmingham, Alabama.
Ushindi
huo wa Wilder ameupata licha ya kuhisiwa kuvunjika mkono wake pamoja
na kuchana misuli ya kwenye mikono wakati wa pambano hilo.
Ngumi nzito ya kushoto ya Deontay Wilder ikimuingia vilivyo Chris Arreola
Deontay Wilder akimpiga konde Chris Arreola licha ya kwenda chini
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni