Raia
wa Tunisia ambaye aliendesha lori na kugonga kundi la watu Jijini
Nice, Ufaransa alifanya utafiti siku kadhaa kabla ya kufanya
shambulizi hilo.
Ripoti
zinasema Mohamed Lahouaiej-Bouhlel aliendesha kwenye barabara ya
kando ya ufukwe wa bahari wa Promenade siku ya jumanne na jumatano
kama maandalizi.
Zaidi
ya watu 80 walikufa kwa kugongwa na lori alilokuwa akiliendesha
wakati wakiwa katika eneo hilo la ufukwe wakisherehekea sikukuu ya
Bastille kwa kuangali fataki, Alhamisi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni