.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 5 Julai 2016

DK. SHEIN AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KATIKA UKUMBI WA IKULU

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba, alipowakumbusha majukumu yao na kuwataka wafanye kazi sheria na taratibi kwa kazi iliyopo sio kufanya kazi kwa mazoea, aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
Washauri wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein wakiwa katika mkutano uliofanywa na Rais kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambao mkutano huo umewataka wakuu hao kutekeleza majukumu yao kama sheria za Utumishi zinavyoeleza na sio kufanya kazi kwa mazoea,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
Baadhi ya Wakuu wa Wilaya za Unguja na Pemba wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyotolewa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja kwa ajili ya kukumbushwa majukumu yao katika maeneo yao kazi,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wakuu wa Mikoa na Wilaya Unguja na Pemba, alipowakumbusha majukumu yao na kuwataka wafanye kazi sheria na taratibi kwa kazi iliyopo sio kufanya kazi kwa mazoea, aliyasema hayo leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,[Picha na Ikulu.] 04/07/2016.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni