Permanent Secretary for the Ministry of Information Communication Technology Hon. Prof. Faustin Kamuzora
Ribbon cut for official launch of Huawei Mlimani City brand shop by Huawei MD. Levin Zhang (Yongquan) Hon. Prof. Faustin Kamuzora Permanent Secretary for the Ministry of Information Communication Technology and Deputy Ambassador of Chinese Embassy Mr. Gou Haodong.
Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Faustin Kamuzora ameipongeza kampuni ya Huawei Tanzania
katika juhudi zake endelevu za kuleta teknologia ya mawasiliano yenye kiwango
cha juu kwa watanzania, kufuatia uzinduzi rasmi wa duka la 7 la bidhaa za
Huawei na kitengo cha huduma kwa wateja katika duka la Mlimani City, Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mapema mwaka huu Huawei Tanzania walianzisha mpango wao wa kuongeza
mtandao wao wa usambazaji nchini kote kwa kuongeza maduka ya bidhaa zao nchini
kote. Uzinduzi wa duka la bidhaa zake la Mlimani City ni mwitikio wa uhitaji
unao ongezeka wa bidhaa za Huawei nchini na kuhakikisha kuwa bidhaa za Huawei
na huduma zake zinapatikana kwa urahisi kwa wateja wa Tanzania.
Tangu mwanzoni mwa mwaka huu Huawei Tanzania imefanikiwa kuzindua maduka
7 ya bidhaa zake na kuongeza idadi ya mawakala wake nchini. Miongoni mwa maduka
hayo ni duka liliolopo Mtaa wa Samora, City Mall na JM Mall jijini Dar es
Salaam na maduka mengine mengi katika mikoa ya Mwanza, Arusha na Mbeya.
Huawei Tanzania inatarajia matokeo mazuri katika duka lake la Mlimani
City na kitengo cha huduma za simu kufuatia mauzo mazuri na huduma
vilivyodhihirishwa na maduka mengine ya Huawei nchini kote.
Duka hili la 7 la
bidhaa za Huawei na kitengo cha huduma kwa wateja la Mlimani City ndilo kinara
cha maduka yote ya Huawei Tanzania. Duka hili linawaahidi watanzania bidhaa na
huduma za ubora wa juu kabisa.
Huawei imekuwa mstari wa
mbele daima katika ubunifu na mabadiliko ya kiteknolojia kwa kwenda sambamba na
mabadiliko na mahitaji ya wateja.
“Tumehakikisha kuwa tunakidhi kila mahitaji ya wateja wetu, hata hivyo
tumeenda mbali zaidi kwa kuzingatia tofauti za vipato vyao na matumizi kwa
kuwaletea bidhaa ambazo zitakidhi haja ya kila mteja wetu”. Alidhihirisha
Mkurugenzi Mtendaji wa Huawei Tanzania
Bw. Levin Zhang (Yongquan), katika hotuba yake ya sherehe ya ufunguzi.
“Huawei Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa
nchini na imejikita katika kuhakikisha ukuaji na maendeleo ya sekta ya
mawasiliano nchini. Tangu kuanzishwa kwa shughuri zetu nchini, tumeshirikiana
na sekta mbalimbali ikiwamo serikali katika kuipeleka mbele TEHAMA.
Huawei
Tanzania imedhamiria kuwa kinara wa simu za kisasa Tanzania, kwa kuwapatia
wateja wake simu bora na zinazotumika kwa urahisi.”
Alidhihirisha mkurugenzi huyo.
Akiwahutubia wananchi wakati wa uzinduzi huo, Katibu Mkuu Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora ambaye ndiye alikuwa
mgeni rasmi aliipongeza kampuni ya Huawei Tanzania kwa hatua waliyoichukua ya
kuinua sekta ya TEHAMA nchini.
Katibu mkuu huyo amepongeza juhudi zilizofanywa
na Huawei Tanzania si tu katika kuleta mawasiliano bora na teknolojia kwa
kupitia bidhaa zao nyingi za simu za kisasa bali pia kwa kuwezesha upatikanaji
wa fursa za ajira kwa watanzania.
“Kwa miaka mingi sasa serikali ya Tanzania
imekuwa na uhusiano mkubwa na Huawei Tanzania, na tumeshirikiana na kampuni hii
katika miradi mingi kwa mafanikio makubwa. Kwa kupitia ubunifu wao katika eneo
la TEHAMA, Huawei imeendelea kuwa na mchango mkubwa kwa nchi yetu.
Ufunguzi wa
duka hili hapa Mlimani City ni hatua ya mwendelezo wa juhudi zake kwa wateja
wake wa Tanzania ambao wanauhitaji mkubwa wa teknolojia ya mawasiliano. Nina
matumaini kuwa kwa kupitia hatua mabalimbali ambazo serikali imechukua katika
kukabiliana na changamoto zinazoikabili TEHAMA na kwa mwendelezo wa ushirikiano
wa wadau binafsi kama Huawei Tanzania, malengo yetu ya Milenia ya kuwawezesha
watanzania kwa kupitia TEHAMA yatafikiwa”.
Alisema Katibu Huyo.
Naibu balozi wa Ubalozi wa
China Bw. Gou Haodong ambaye alishiriki sherehe za uzinduzi ameipongeza Huawei
Tanzania kwa hatua yake muhimu ya kuboresha sekta ya mawasiliano ya simu
nchini.
“Nina matumaini kuwa kampuni hii kubwa kutoka China
itaendelea kuwekeza katika sekta ya mwasiliano hapa Tanzania. Naamini, kwa
juhudi za pamoja baina ya serikali na Huawei zitaifanikisha Tanzania kuifikisha
sekta hii katika viwango vya juu”. Alisema
Serikali ya Tanzania inatambua mchango wa Huawei
katika kuhakikisha upatikanaji wa simu halisi hapa nchini. Kampuni hii pia
imeendesha miradi kadha wa kadha ya kuendeleza vipaji vya TEHAMA nchini ambayo
imewajengea uzoefu wnafunzi wa kitanzania na kuwaandaa kufanya kazi katika
makampuni ya simu. Huawei pia imeteuliwa kuwa mshauri wa serikali wa TEHAMA,
mradi ambao utaipa nafasi Huawei ya kutoa mafunzo ya TEHAMA, elimu na huduma
kubwa za data.
Katika kusherehekea uzinduzi huu wa duka la bidhaa
za Huawei Mlimani City, Huawei Tanzania inatoa punguzo maalum kwa aina kadhaa
za simu kuanzia Julai 16 hadi 31. Huawei pia imetangaza uwepo wa tolea lake
jipya kabisa lenye teknolojia ya juu zaidi la Huawei P9 katika soko la
Tanzania.
P9 ni simu ya kwanza duniani yenye kamera mbili, inayounda picha
zenye kiwango cha juu kabisa. Kila bidhaa ya Huawei imekuwa ikibadili ubora
katika ulimwengu wa simu katika hadhi na utendaji wake. Huawei P9 imeundwa kwa
ajili ya kuleta mapinduzi ya upigaji wa picha kwa simu katika viwango vipya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni