Indonesia
imethibitisha kuwa itatekeleza adhabu ya kifo kwa watu 14,
waliohukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya dawa za kulevya wakiwemo
waafrika katika siku za hivi karibuni.
Maafisa
wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa wameelezea hofu yao kuhusiana
na mpango huo na kuitaka serikali ya Indonesia kukomesha adhabu hiyo
ya kifo ambayo haitendi haki.
Wafungwa
hao waliohukumiwa adhabu ya kifo majina yao hayajatajwa, lakini
imefahamika kuwa wamo raia wa Nigeria, Zimbabwe, Pakistan pamoja na
India.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni