Kiungo
wa Chelsea Cesc Fabregas ameonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu
mchezaji mpya wa Liverpool Regnar Klaven katika mchezo wa kirafiki
uliofanyika nchini Marekani.
Katika
mchezo huo wa jana usiku Chelsea iliibuka na ushindi wa goli 1-0,
goli lililofungwa kwa kichwa na beki Gary Cahill katika dakika ya 10
ya mchezo kufuatia kona iliyopigwa na Fabregas.
Cesc Fabregas akimchezea rafu Regnar Klaven huku refa akimuangalia
Gary Cahill akiruka juu angani na kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Fabregas na kuandika goli pekee katika mchezo huo
Baadhi ya wachezaji wa Chelsea wakishangilia pamoja na Cahill goli alilofunga
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni