Rais
wa Marekani Barack Obama amewasihi wapiga kura kuendelea kumuunga
mkono kwa kufanikisha Bi. Hillary Clinton kushinda katika uchaguzi
mkuu wa rais Novemba.
Obama
amemsifia Bi. Clinton katika mkutano wa taifa wa chama cha Democratic
huko Philadelphia, kwa kusema ni mtu mwenye sifa zaidi kuwahi
kugombea kuingia Ikulu ya Marekani.
Amewaambia
wapiga kura kuwa wanakabiliwa na chaguo baina ya matumaini ama hofu
na mashambulizi yanayojengwa na mgombea wa Republican Donald Trump.
Rais Barack Obama akikumbatiana na Bi. Hillary Clinton baada ya kumaliza hotuba yake
Bi. Clinton akiwa na furaha tele akiwapungia mkono wajumbe wa Democratic akiwa na rais Barack Obama
Rais Barack Obama akimyanyua mkono juu Bi. Hillary Clinton huku akiwapungia mkono wajumbe wa chama cha Democratic
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni