Maandalizi
ya fainali ya Euro 2016 baina ya Ufaransa na Ureno yaligubikwa na
tukio la kuvamiwa na kundi la wadudu jamii ya vipepeo waliosababisha
bughudha kwa watu mbalimbali.
Wachezaji
na mashabiki walilazimika kulikwepa kundi hilo la maelfu ya jamii ya
vipepeo lililokuwa likiruka katika maeneo mbalimbali ya dimba la
Stade de France Jijini Paris.
Cristiano Ronaldo akionekana kukerwa na wadudu hao jamii ya vipepeo
Collina akionyesha kukerwa na hali hiyo ya kujaa uwanjani kwa wadudu hao jamii ya vipepeo
Beki Pepe akitumia mkono wake kuwapangusa wadudu hao jamii ya vipepeo waliovamia uwanjani.
Maafisa wa benchi la ufundi la Ufaransa wakihangaishwa na wadudu hao jamii ya vipepeo
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni