Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa pande zinazokinzana
Sudan Kusini kusitisha mara moja mapigano yaliyoibuka hivi karibuni,
na kuzuia kusambaa kwa machafuko.
Katika
taarifa yake, baraza hilo limeshutumu vikali mapigano hayo, kwa kauli
nzito na kuonyesha kushtushwa pamoja na kukerwa na mashambulizi
yaliyofanywa katika maeneo ya Umoja wa Mataifa.
Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetaka kuongezwa kwa idadi zaidi
ya walinda amani, huku mamia ya watu tayari wakiwa wamesharipotiwa
kuuwawa tangu kuibuka kwa mapigano hayo mapya siku ya Ijumaa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni