.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Julai 2016

JIJI LA LISBON NA VIUNGA VYAKE LATIKISWA KWA SHAMRASHAMRA ZA UBINGWA WA EURO 2016

Jiji la Lisbon jana usiku lilijawa na shamrashamra, wakati makumi kwa maelfu ya mashabiki wa Ureno walipokuwa wakirandaranda mitaani wakipiga honi za magari na kuwasha jope kushangilia ubingwa wa Euro 2016.

Shamrashamra hizo zilisambaa zaidi pale kapteni wa Ureno Cristiano Ronaldo alipokabidhiwa kombe la ubingwa huo wa kwanza kimataifa kwa taifa hilo, ambalo lilikuwa halipewi nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo.
   Mashabiki wa Ureno wakiwa wamepagawa kwa ubingwa wakifuatilia matokeo kwa kutumia luninga kubwa
             Mitaani pia magari yalirandaranda yakipiga honi kusherehekea ubingwa
                            Ni furaha tele Lisbon nchini Ureno kama inavyoonekana hapa 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni