Ureno
wameweza kuishinda hofu ya kumpoteza kapteni wao Cristiano Ronaldo na
kuwafunga wenyeji Ufaransa katika fainali ya Euro 2016, ikiwa ni
ushindi wao wa kwanza wa taji la kimataifa, shukurani kwa Elder
aliyefunga goli pekee katika muda wa nyongeza.
Mshambuliaji
nyota wa Real Madrid, Ronaldo ambaye pia ni kapteni wa Ureno
aliondolewa uwanjani kwa kubebwa kwenye machela katika dakika ya 25
tu ya mchezo huo katika dimba la Stade de France Jijini Paris, ikiwa
ni dakika nane tu baada ya kuumia goti lake baada kugongana na
Dimitri Payet.
Wenyeji
Ufaransa waliokuwa wakipewa nafasi kubwa ya kushinda walishindwa
kutumia fursa ya Ureno kumkosa Ronaldo baada ya dakika ya 25, ingawa
walikuwa karibu washinde wakati wa kumalizika dakika tisini za
kawaida pale Andre-Pierre Gignac alipoachia shuti lililogonga mwamba
kwa ndani.
Elder aliyetokea benchi akiachia shuti kali na kuandika goli pekee la ushindi katika fainali ya Euro 2016 mnamo dakika ya 109
Wachezaji wa Ureno wakimkumbatia Elder baada ya kufunga goli lililoandika historia mpya kwa Ureno
Ronaldo akimwaga chozi la furaha huku akiwa ameshika kichwa kwa mshangao baada ya Ureno kufunga goli lililowapa ushindi
Cristiano Ronaldo akitolewa nje akiwa amebebwa baada ya kuumia goti katika dakika ya 25
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni