Kocha Jose Mourinho ameanza harakati
za kutenga dau kubwa ili kumshawishi Paul Pogba kuhamia Manchester
badala ya Real Madrid ambayo nayo inamuwania.
Marafiki wake wa Juventus na
Ufaransa wamesema kuwa Pogba angependelea kwenda Real Madrid kuliko
kurejea tena Manchester United.
Hata hivyo, Manchester United
inaamini kuwa Real Madrid haijaamua kuvunja benki ili kumnunua Pogba
kwa ada itakayoweka rekodi.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni