Mkurugenzi wa kitengo cha Africa wa JICA, Hideki Watanabe akielezea Jinsi JICA wanavyofanya shughuli za Maendeleo Afrika
Mkurugenzi wa Namaingo Bi.Ubwa Ibrahim akimwelezea jambo mwakilishi wa benki ya rasilimali (TIB) walipokutana katika semina ya uwezeshaji mitaji kwa ajili shughuli za maendeleo.
Watoa mada kutoka mashirika na taasisi mbalimbali za kifedha wakijibu maswali kutoka kwa wadau waliohudhuria semina hiyo.
Wajasiriamali wakubwa kwa wadogo wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia fursa zilizopo ili waweze kuwezeshwa mitaji ili wawekeze katika shughuli za maendeleo ili kupunguza tatizo la ajira hapa nchini
na kusaidia juhudi za serikali na wadau kuleta maendeleo hapa nchini.
na kusaidia juhudi za serikali na wadau kuleta maendeleo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Balozi wa Japan hapa nchini Bwana Masaharu Yoshida alipokua akifungua semina ya wadau wa maendeleo iliyojadili uwezeshaji wa mitaji kwa wajasiriamali kwa ajili ya shughuli za maendeleo iliyofanyika jana (5/6/2016) jijini Dar es Salaam.
Semina hiyo iliyoandaliwa na shirika la ushirikiano na maendeleo la Japan (JICA) pamoja na taasisi ya sekta binafsi hapa nchini (TPSF) ilihudhuriwa na mashirika na taasisi za kifedha pamoja na wajasiriamali kutoka sekta binafsi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, watoa mada walionesha kuwa kuna fursa kubwa kwa watanzania wote walioamua kuwa wajasiriamali kwa kufungua viwanda vidogo kwa vikubwa, wakulima na wafanyabiashara kutumia mashirika na taasisi za fedha kujipatia mikopo nafuu ili kuwezesha kukuza biashara na viwanda vyao na wanaweza kulipa kwa muda mrefu
kwa riba nafuu.
kwa riba nafuu.
Semina hiyo ilibainisha kuwa changamoto kubwa ni kutokua na taarifa kwa watanzania wengi na hivyo kuogopa kuwekeza kwa kutumia taasisi za fedha jambo lililoungwa mkono na washiriki wengi kwani imebainika kuwa ni asilimia 16 tu ya watanzania wanatumia huduma za kibenki
hivyo wameaswa kubadilika waweze kunufaika na mitaji ambayo ipo lakini hakuna wanaokidhi vigezo ambapo wanaofuatilia na kunufaika ni watu wachache.
hivyo wameaswa kubadilika waweze kunufaika na mitaji ambayo ipo lakini hakuna wanaokidhi vigezo ambapo wanaofuatilia na kunufaika ni watu wachache.
Mwavuli wa wajasiriamali wa Namaingo (Namaingo Business Agency) ni moja ya taasisi zilizohudhuria na ziliahidiwa kupewa ushirikiano na wadau wote wa kuwasaidia kufikia malengo yao kwani mitaji ipo na Namaingo inakidhi vigezo vyote vya kukopesheka kwani mpango kazi wake uko kitaalamu na ushiriki wa serikali na taasisi zake unaifanya iwe mkombozi kwa watanzania wengi maskini.
Akizungumza baada ya semina hiyo Mkurugenzi wa taasisi hiyo Bi. Ubwa Ibrahim aliwataka watanzania wote wajitokeze kujiunga na taasisi yake wawekwe katika mpango wa kuwarasimisha na kuwawezesha kuingia
katika mipango ya kuwainua kiuchumi kwani kuna mradi wa kijiji biashara ambacho wanachama wanatarajia kukopeshwa ardhi, kujengewa nyumba za makazi, kukopeshwa mradi uliokamilika (kilimo na ufugaji) pamoja na utaalamu na usimamizi wa mradi husika.

“Kwa sasa tuko katika hatua ya utekelezaji ambapo tarehe 28 mwezi huu tunasaini mikataba na serikali na wadau wengine Diamond Jubilee. Naomba watanzania waje washuhudie na kusikia juu ya mradi ili waamini
maanake kuna watu wanaongea bila kutenda, mimi nawakaribisha waje waone utendaji na tuwape ushuhuda wa hatua tulizokia kwenye mradi wetu wa kijiji biashara ambapo serikali imetoa ekari 44,000 kwa ajili ya mradi huu. Maendeleo hayakusubiri hivyo kila mtu achangamke aje atuone tumweke kwenye mpango rasmi” alisema Bi.Ubwa.

Mwanasheria wa taasisi hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Bwana Payas alisema kila siku kuna mafunzo katika vituo vya Namaingo vilivyopo Ubungo, Ukonga na Temeke ambapo alisema wajasiriamali hupewa mafunzo kabla ya kuingizwa rasmi katika mpango wa kampuni.
“Namaingo tunawezesha wajasiriamali kusajiliwa TRA, BRELA, TFDA, Bima ya afya, mifuko ya jamii na kuwaunganisha wao kwa wao. Kila Jumamosi tunakaribisha wanachama wapya wanaopewa maelekezo na kuelezwa juu ya mradi wetu mkubwa wa kijiji biashara kilichopo Mbawa, Rufiji ambapo Namaingo inaratibu mradi huo pamoja na wadau wa maendeleo tukisimamiwa na baraza la uwezeshaji chini ya ofisi ya waziri mkuu”
aliongeza.
aliongeza.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni