Kaka
wa mwanamke wa Pakistan aliyejizolea umaarufu kwenye mitandao ya
jamii amesema amemuuwa dada yake huyo baada ya kugoma kuacha kutuma
picha na video zenye kuwatega wanaume kwenye Facebook.
Kaka
huyo Muhammad Waseem amesema kuwa hajisikii aibu kwa kumuua dada yake
huyo Qandeel Baloch licha ya mauaji hayo kuibua mjadala wa kitaifa
dhidi ya wimbi la mauaji ya kulinda heshima nchini Pakistani.
Muhammad Waseem akiwa mikononi mwa polisi kwa mauaji ya dada yake
Mama wa marehemu Qandeel Baloch, akiangua kilio mbele ya mwili wa binti yake
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni