Maafisa
polisi watatu wameuwawa kati ya sita waliopigwa risasi na mtu mwenye
bunduki aliyefunika sura yake, huko Baton Rouge Marekani, ikiwa ni
chini ya wiki mbili tangu kuuwawa kwa mtu mweusi Alton Sterling
katika mji huo huo wa Lousiana.
Mwanaume
aliyekuwa amevalia mavazi meusi alifyatua risasi hovyo majira ya saa
tatu asubuhi, akiwa anatembea katika eneo la duka na eneo la kuogeshea
magari kwa mujibu wa mashahidi wa tukio hilo.
Polisi
waliarifiwa kwa simu ya 911 kuhusiana na kuonekana mtu anayeranda na
silaha eneo hilo, na inaaminika mtu mmoja aliyekuwa na silaha
aliwafyatulia risasi polisi walipowasili.
Polisi
wamesema mtuhumiwa mmoja mwenye silaha amepigwa risasi na kufa na
kuongeza kuwa watuhumiwa wengine wawili hawajulikani walipokimbilia
baada ya kushambuliwa na polisi.
Polisi wakiwa katika hali ya taharuki baada ya wenzao kuuwawa huko Baton Rouge
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni