Kuingia huko mkataba wa udhamini wa miaka nane kati ya CAF na Total, kunakuja baada ya mdhamini wa awali kampuni ya simu ya Orange na Shirikisho hilo la mpira wa miguu barani Africa kumalizika.
Total watakuwa wadhamini wakuu katika michuano ifuatayo:-
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika
- Ligi ya Klabu Bingwa Afrika
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
- Super Cup ya Afrika
- Kombe la Mashirikisho
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika kwa Wanawake
- Kombe la Futsal Afrika
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20
- Kombe la Taifa Bingwa Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni