Video
inayomuonyesha mmoja wa wanamuzika maarufu barani Afrika Koffi
Olomide, akimpiga mwanamke katika uwanja wa Kimataifa wa Jomo
Kenyatta imesambaa mitandaoni.
Mwanamuziki
huyo wa DR Congo anaonekana kwenye video hiyo akimpiga teke mwanamke,
anayesemekana kuwa ni mcheza shoo wake wa bendi ya Quartier Latin,
mbele ya abiria wengine na polisi wakati walipowasili kwenye uwanja
huo.
Licha
ya kufanya kitendo hicho cha kupigana hadharani, Koffi Olomide ambaye
yupo nchini Kenya kwa ajili ya kufanya shoo mwishoni mwa wiki hii
polisi hawakumkamata, na hadi sasa haijatolewa taarifa yoyote
kuhusiana na tukio hilo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni