Bondia Idd Mkwela kushoto akiwa na Mwita Machage baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya julai 24 katika ukumbi wa musoma bar Tandika Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila'Super D' wa pili kushoto akiwa na mabondia Idd Mkwela kushoto Vicent Mbilinyi Shabani Kaoneka na Mohamed Kisua
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akiwa na mabondia wake Mohaed Kisua kg 51 iDDi Mkwela kg 61 Vicent Mbilinyi Kg 63 na Shabani Kaoneka Kg 72 Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
BONDIA Idd Mkwela atapanda tena ulingoni kesho jumapili katika mpambano wake mwingine wa Kg 61 atakapo mkabili Mwita Machage katika ukumbi wa musoma bar uliopo tandika
Akizungumza baada ya upimaji uzito na afya kwa mabondia watakaocheza siku hiyo
Rais wa oganaizesheni ya ngumi za kulipwa TPBO Yassin Abdallah 'Ostadhi' amesema kuwa mabondia wengine waliopima na watagombania ubingw wa taifa ni Imani Mapambano atakaezichapa na Selemani Galile raundi kumi za ubingwa
kKatika mapambano haya tumeamua kuchukuwa mabondia chipkizi kwa ajili ya kuendelea kuamasisha mchezo wa ngumi sehemu mbalimbali nchini
hususani katika ukanda uhu wa Temeke ambapo tumekuwa tukichezesha vijana wanao chipukia kila wakati
Katika Mchezo huo kutakua na Uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni