.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 23 Julai 2016

MAMBO YAMENOGA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM MJINI DODOMA.

                                           Ni burudani kutoka kwa bendi ya TOT Pus Ukumbini
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa mwongozo wa kuanza kwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma.
                                                                                                         Taswira UkumbiniWajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia), akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Igoma Jijini Mwanza, wakiwa katika Viunga vya Ukumbi mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma wa Dodoma Convetional Centre ambapo Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unafanyika.

Ni Mkutano Maalumu kwa ajili ya Wajumbe hao kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa, ambapo jana Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipitisha kwa kura zote jina la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa chama hicho. Dkt.Magufuli anapokea kijiti cha uongozi wa chama kutoka kwa Rais Mstaaf wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

Mji wa Dodoma umegubikwa na shamra shamra mitaa yote na tayari wajumbe wa Mkutano Mkuu wameanza kuingia Ukumbini kwa ajili ya Mkutano huo huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa vyema kila kona.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akisalimiana na mjumbe mwenzake wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leo
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto) akiwa na Katibu wake, Heri James, Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leo
Heri James (kushoto) akiwa na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, wakisalimiana ukumbini.
Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto), akiwa ukumbini na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.
Kaimu Katibu wa CCM mkoani Mwanza Elias Mpanda (kulia) akisalimiana na aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Manju Msambya (kushoto)
Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM akiwemo Le Mutuz (kulia) wakiperuzi taarifa mbalimbali kuhusiana na Mkutano huo.
Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa burudani na Bendi ya TOT Pus


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni