Baada ya kupita miezi miwili tangu
machinjio ya nyama ya punda yaliyogharimu shilingi milioni 300 za
Kenya kuanza kazi, bado hawajafanikiwa kusafirisha shehena ya kwanza
ya nyama za punda kutokana na upatikanaji mdogo wa punda.
Waziri wa Kilimo Kenya Willy Bett
alizindua machinjio hayo Aprili mosi mwaka huu, kwa lengo la kuuza
nyama hizo za punda katika masoko ya China na Urusi pamoja Mashariki
ya Mbali ambako nyama ya punda inahitajika sana.
Ili kufikia mahitaji ya soko hilo
machinjio hayo yanahitaji kufikia mahitaji ya kusafirisha tani 100
hadi 200 za nyama ya punda katika mataifa hayo, ambapo kwa siku
walipanga kuchinja punda 100.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni