Mwanariadha
Usain Bolt atatetea ubingwa wake wa Olimpiki wa mbio za mita 100, 200
pamoja na mbio za kupokezana vijiti baada ya kutajwa kwenye kikosi
cha Jamaica kitakachoenda Rio.
Kulikuwa
na hofu ya uwezekano wa Bolt kushiriki michuano hiyo ya Olimpiki
nchini Brazil kutokana na kuwa na majeraha katika misuli yake ya
mguuni, kiasi cha kushindwa kufanya majaribio ya kufuzu katika timu
ya taifa.
Hata
hivyo bingwa huyo mara sita wa michuano ya Olimpiki kwa mita 100 na
200 na ambaye anashikilia rekodi ya dunia ametajwa kwenye kikosi cha
wachezaji 63 wa timu ya taifa ya Jamaica.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni