Marekani
imesema mapigano yaliyoibuka na kusababisha vifo vya mamia ya watu
nchini Sudan Kusini lazima yasitishwe.
Ikulu
ya Marekani imeonya kuwa mtu yeyote atakayejaribu kukwamisha jitihada
za kusimamisha mapigano atawajibika.
Umoja
wa Mataifa umetaka kuwekwa mara moja vikwazo vya silaha kwa nchi
hiyo, na kutumika helkopta zenye kushambulia ili kuimarisha amani.
Mapigano
ya tangu Ijumaa baina ya vikosi vitiifu kwa rais Slava Kiir na vya
Makamu wa rais Riek Machar katika jiji la Juba yamesababisha vifo vya
mamia ya watu.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni