Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kesho Jumamosi Julai 30, 2016
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa mashindano ya kuibua
na kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume ulioko kwenye makutano ya Barabara za Uhuru na Shaurimoyo,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Sambamba
na Makonda, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Jamal Malinzi naye amethibitisha kuwako kwenye hafla hiyo ambayo
mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za Ilala Boys dhidi ya Bombom
Ilala, Dar es Salaam. Inawakilishwa na mikoa yote mitatu kisoka
ambayo ni Ilala, Kinondoni na Temeke kwa pande zote mbili za wavulana
na wasichana.
Kadhalika,
wakuu wa mikoa mingine ambayo mashindano hayo yatafanyika nao
watakuwa wageni rasmi katika mikoa yao ambayo ni Mbeya, Mwanza na
Morogoro kwa upande wa wavulana pia Arusha, Lindi na Zanzibar kwa
upande wa wasichana.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni