Timu
ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17
ya Madagascar kesho Jumamosi Julai 30, 2016 itacheza mchezo wa
kirafiki wa kimataifa dhidi ya Serengeti Boys ya Tanzania kwenye
Uwanja wa Taifa wa Madagascar.
Serengeti
Boys imepiga kambi jijini Antananarivo, Madagascar kujiandaa kucheza
na Afrika Kusini katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6, 2016.
Mchezo wa marudiano utafanyika Agosti 21, mwaka huu kwenye Uwanja wa
Azam, ulioko Chamazi-Mbagala, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Taarifa
kutoka kwa mkuu wa msafara Ayoub Shaibu Nyenzi ambaye ni Mwenyekiti
wa Kamati ya Soka la Vijana, zinasema mchezo huo ni muhimu na Kocha
Kocha Mkuu, Bakari Nyundo Shime au Mchawi Mweusi, amesema kwamba
amefurahi kupata nafasi hiyo huku Daktari wa timu hiyo, Shecky
Francis Mngazija akithibitisha kwmaba vijana hao wako salama.
Nyota
walioko kambini ni pamoja na makipa, Ramadhani Awm Kabwili, Kelvin
Deogratius Kayego na Samwel Edward Brazio wakati mabeki wako Kibwana
Ally Shomari, Nickson Clement Kibabage, Israel Patrick Mwenda,
Dickson Nickson Job, Ally Hussein Msengi, Issa Abdi Makamba na Enrick
Vitalis Nkosi.
Viungo
ni Kelvin Nashon Naftal, Ally Hamisi Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali,
Syprian Benedictor Mtesigwa, Ibrahim Abdallah Ali, Shaban Zuberi Ada
huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Abdallah Rashid, Yohana Oscar
Mkomola na Muhsin Malima Makame.
Serengeti
Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli
kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa. Mshindi
wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu
mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.
Hivi
karibuni Serengeti Boys ilifanya ziara India ambako walishiriki
mashindano ya vijana ya Kimataifa yanayotambuliwa na FIFA (AIFF
International Youth Tournament 2016) kabla ya kurudi na rekodi ya
kupigiwa mfano si tu katika Tanzania na kwa nchi za Afrika Mashariki.
Ilishika nafasi ya tutu nyuma ya Korea Kusini na Marekani.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni