Mapigano
mapya yameibuka Sudan Kusini baina ya vikosi vitiifu kwa rais pamoja
na vile vya makamu wa rais.
Ripoti
kutoka Jijini Juba zinasema kumesikika milio ya risasi na milipuko
mikubwa katika maeneo yote ya Jiji hilo, kuashiria kutumika kwa
silaha nzito.
Zaidi
ya watu 200, wameripotiwa kufa katika mapambano hayo yaliyoibuka
tangu Ijumaa. Mapigano hayo mapya yamekuja wakati Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa lilizionya pande mbili kusitisha mara moja
mapigano.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni