.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 11 Julai 2016

MABINGWA WA EURO 2016 WAPOKELEWA KISHUJAA NA MAELFU YA WATU JIJINI LISBON

Maelfu ya mashabiki wamejipanga katika mitaa ya Jiji la Lisbon nchini Ureno kuwakaribisha wachezaji wao mashujaa waliowafunga Ufaransa goli 1-0 katika fainali ya Euro 2016.

Wakati ndege iliyowabeba timu hiyo inatua nchini Ureno, ilipokelewa kwa moshi wenye rangi nyekundu na kijani, rangi ambazo ni za bendera ya taifa la hilo.
Ndege iliyobeba timu ya taifa ya Ureno ikirushiwa moshi mwekundu na wa kijani ikiwa ni sehemu ya shamrashamra za mapokezi
Mabingwa wa Euro 2016 timu ya taifa ya Ureno wakiwa katika picha ya pamoja ndani ya ndege iliyowarudisha
Mashabiki wakiwapokea kwa shangwe mashujaa wao kwa kuwapungia mikono na kuwashangilia katika Mitaa ya Jiji la Lisbon

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni