Michelle
Obama mke wa rais wa Marekani amemponda mgombea urais wa Republican
Donald Trump, na kumuunga mkono Hillary Clinton katika mkutano wa
Taifa wa Chama cha Democratic huko Philadelphia.
Huku
akishangiliwa na kupigiwa makofi na wajumbe wa mkutano huo Michelle
Obama amesema lugha za chuki zinazotolewa na watu mashuhuri kwenye
TV, haziwasilishi moyo wa uzalendo wa taifa hilo.
Kama
hiyo haitoshi Michelle amewataka wafuasi wa chama cha Democratic
kutojishusha sawa na wapinzani wao, kwani kauli mbiu ya chama hicho
ni “Wao wakijishusha, sisi tunakwenda juu”.
Awali
aliyekuwa mshindani mkuu wa Bi. Clinton, Seneta Bernie Sanders
amewasihi wafuasi wa chama cha Democrat, kumuunga mkono Bi. Hilary
Clinton.
Wanachama wa Democrat wakimshangilia Michelle Obama wakati akitoa hotuba yake
Michelle Obama akionyesha ishara ya vidole gumba baada ya kumalizi kutoa hotuba yake
Rais Obama alishindwa kujizuia na kutuma twitti ya kumfagilia mkewe Michelle Obama kwa hotuba nzuri aliyoitoa
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni