Mmoja
wa watalii wapanda Mlima Kilimanjaro katika msafara maalum wa Afrika
Kusini ujulikanoa kama Trek4Mandela, aitwae Gugu Zulu amepoteza
maisha yake wakati akipanda kileleni mwa Mlima huo leo asubuhi.
Gugu
ambaye ni mtu maarufu nchini Afrika Kusini pia ni dereva wa mbio za
magari alikuwa ameambatana na mkewe Letshengo katika msafara huo
ambao huandaliwa na taasisi ya Nelson Mandela.
Taarifa
zilizotolewa zinaeleza kuwa Gugu alipata matatizo ya kushindwa
kupumua, ambapo timu ya matibabu walimwekea dripu na kushuka naye
chini ya Mlima, na walijaribu kila wawezalo kuokoa maisha yake lakini
ikashindikana.
Marehemu Gugu Zulu akiwa na mkewe Letshengo pamoja na mtoto wao
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni